Na: Stephano Simbeye, Mbozi
Mahakama ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe
imemhukumu kifungo cha miaka saba
gerezani mwanamke mmoja mkazi wa Majengo
katika halmashauri ya Tunduma, Happness Mwakisyala(28) baada ya kukiri kutaka
kuiba mtoto wa kiume mwenye umri wa saa 12 katika hospitali ya serikali ya
wilaya (Vwawa) kinyume cha kifungu cha sheria 169 (1) b sura ya 16 kanuni ya
adhabu kama ilivyofanyiowa marekebisho mwaka 2002.
Akisoma hukumu mara baada ya mshitakiwa kukiri mahakamani
hapo, hakimu wa mahakama hiyo Nemes
Chami alisema kwa kuwa mshitakiwa amekiri yeye mwenyewe kutenda kosa hilo na
kwa kuwa vitendo kama hivyo vinaanza kukithiri kwenye jamii, mahakama yake
inamhukumu kifungo cha miaka saba gerezani ili iwe fundisho kwa wengine wenye
nia kama hiyo.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka Samwel
Siro kuwa mshitakiwa huyo kwa makusudi aliingia kwenye wadi ya wazazi katika
hospitali ya serikali ya wilaya, na kumuiba mtoto wa kiume na kwenda kumficha
chooni kabla ya kuondoka naye.
Siro alidai kuwa tukio hilo lilitokea Mei 11 mwaka huu saa
11alfajiri katika hospitali hiyo na kumwiba mtoto mchanga.
Mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama kutoa adhabu kari
kwa mshitakiwa kutokana na vitendo vya kuiba watoto kukithiri hivi sasa ili iwe
fundisho kwa wengine wenye nia kama hiyo.
Aidha mshitakiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea ili
mahakama iweze kumuonea huruma kabla ya kutoa hukumu alisema “ ni kweli
nilitenda kitendo hicho naiomba mahakama inihurumie na kunisamehe” alisema
Mwisho.
No comments:
Post a Comment