Social Icons

Sunday, 25 September 2016

Padre Awkakumbusha waumini Kufanya kazi

Na: Stephano Simbeye - VWAWA: Watanzania wametakiwa kuukataa umasikini kutokana na uzembe wa kutofanya kazi, badala yake wajitoe muda wao wote kwa kufanya kazi ambayo itawapatia kipato na mwisho wa siku wataweza kuondokana na umasikini. Kauli hiyo imetolewa leo (jana) na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Patrick Vwawa, wilayani Mbozi mkoni Songwe William Gombanila alipokuwa anahubiri katika misa takatifu ya Jumapili ambapo alisema fursa pekee iliyopo kwa watanzania ni amani na utulivu hivyo itumike kufanya kazi kwa bidii ili kuutokomeza umasikini . Gombanila aliwaasa waumini wa kanisa hilo pia kutumia wakati wao vizuri hasa katika kipindi hiki cha maandalizi ya kuelekea msimu wa kilimo kwa kuandaa mashamba ili mvua zitakapoanza kunyesha wapande badala ya kuzembea wakisubiri mvua ndipo waanze kuandaa mashamba na kwamba wakumbuke kwa kufanya hivyo ni kujichelewesha wenyewe. “ ndugu zangu umasikini upo lakini tuukatae kwa kufanya kazi isije ikawa wewe umeridhika na hali yako wakati wenzako wanaandaa mashamba kipindi hiki wewe umekaa kimywa, au unalima kieneo kidogo nawe unajitapa kwa watu kuwa umelima, unafika wakati wa mavuno huna kitu, jambo hilo ni kujidanganya na mwisho wa siku utajikuta unaishia katika umasikini jambo ambalo ni baya”alisema Padre Gombanila Akizungumzia tofauti ya kipato kati ya walio nacho na wasio nacho alisema hilo limekuwa likitokea tangu enzi za Yesu kuwapo hapa dunini lakini aliwaasa watu kusaidiana kwa kuwa wapo wengine ni wahitaji hivyo kwa aliyenacho asisite kumsaidia asiyenacho ili wote waishi kwa amani na utulivu. Jonasi Mwazembe alisema mahubiri ni mazuri yanamkumbusha kila mmoja wajibu wake na pia umuhimu wa kusaidia walio masikini badala ya kuwaacha wateseke kama masikini Lazaro. Magreth Mwaluanda mahubiri hayo yamemgusa licha ya kuwa padre alifupisha hata hivyo amesema yana fundisho kubwa kwa watu kuwa na moyo wa kujitolea kusaidia wasiojiweza na kwamba si lazima mtu awe na kitu kikubwa ndiyo asaidie Mwisho

No comments:

Post a Comment