Stephano Simbeye, Mbozi
Idara ya afya ya halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, imeshauriwa kuunganisha kampeni zake za kiafya kwa pamoja ili kurahisisha matumizi ya rasilimali chache zilizopo, ili zilete tija.
Ushauri huo umetolewa jana na mkuu
wa wilaya ya Mbozi John Palingo wakati alipotembelea moja ya kituo cha
chanjo katika zahanati ya serikali ya Mlowo, kuwa ili jukabiliana na
changamoto ya ukosefu wa vitendea kazi kama magari ni vyema kampeni mbalimbali
zikafanywa pamoja ili rasilimali hizo chache zitumike vizuri.
"Kampeni mnazofanya kama vile
damu salama huduma za tiba kwa mkoba na nyingine nyingi zifanywe kwa
pamoja"alisema mkuu huyo wa wilaya.
Kauli hiyo ilifuatiwa na kauli ya
mganga mkuu wilayani hapa Dr. Janeth Makoye kueleza changamoto inayokwamisha
shyghuli za chanjo kuwa ni pamoja na ukosefu wa vyombo vya usafiri,majokofu na
upungufu wa dawa za chanjo hasa uliojitokeza mwaka jana. Alisema wilaya Mbozi
ina jumla ya vituo vya kutolea chanjo 62 lakini kati ya hivyo 44 ndivyo
vinafanyakazi hivyo kulazimika jutoa huduma kwa kutumia kliniki inayotembea.
Aidha Dr. Makoye akizunfumzia chanjo
alisema mwaka jana walifikiwa watoto 16927 kati ya watoto 18808 waliokuwa
wamekusudiwa ambayo ni sawa na asilimia 90 na kuwa katika mwaka huo hapakuwepo
na taarifa za magonjwa yaliyojitokeza ambayo yanazuilika kwa njia ya chanjo.
Aliongeza kuwa kuanzia Januari hadi Machi
mwaka huu wamewafikia na kuwapatia chanjo watoto 4806 kai ya watoto 4905 sawa
na asilimia 98 ya lengo kwa kipindi hicho kwa kuwachanja kwa magonjwa dhidi ya
Surua, pepopunda, porio, kifaduro, donda koo, homa ya ini, homa ya uti wa
mgongo na kichomi na kuwa kauri mbiu inasema "Jamii iliyochanjwa ni jamii
yenye afya bora"
mmoja wa akina mama aliyefika
kupatia chanjo mwanae Ezra Njowela alisema kujitokeza kupata chanjo hiyo
kunatokana na mafunzo wanayopata tangu uja uzito wanapohudhuria kliniki, hali inayofanya
kujua umuhimu wa kuhudhuria kliniki na umuhimu wa chanjo, hivyo kutambua faida
za kuwachanja watoto wao na hasara ya kutochanja.
mwisho
No comments:
Post a Comment