Idara ya afya ya halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, imeshauriwa kuunganisha kampeni zake za kiafya kwa pamoja ili kurahisisha matumizi ya rasilimali chache zilizopo, ili zilete tija.
Ushauri
huo umetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Mbozi John Palingo wakati
akifanya uzinduzi wa chanjo kiwilaya uliofanyika katika zahanati ya
serikali ya Mlowo, kuwa ili jukabiliana na changamoto ya ukosefu wa
vitendea kazi kama magari ni vyema kampeni mbalimbali zikafanywa pamoja
ili rasilimali hizo chache zitumike vizuri.
"Kampeni mnazofanya kama vile damu salama huduma za tiba kwa mkoba na
nyingine nyingi zifanywe kwa pamoja"alisema mkuu huyo wa wilaya.
Kauli hiyo ilifuatiwa na kauli ya mganga mkuu wilayani hapa Janeth
Makoye kueleza changamoto inayokwamisha shyghuli za chanjo kuwa ni
pamoja na ukosefu wa vyombo vya usafiri,majokofu na upungufu wa dawa za
chanjo hasa uliojitokeza mwaka jana.
Alisema wilaya Mbozi ina jumla ya vituo vya kutolea chanjo 62 lakini
kati ya hivyo 44 ndivyo vinafanyakazi hivyo kulazimika jutoa huduma kwa
kutumia kliniki inayotembea.
Aidha
Dr. Makoye akizunfumzia chanjo alisema mwaka jana walifikiwa watoto
16927 kati ya watoto 18808 waliokuwa wamekusudiwa ambayo ni sawa na
asilimia 90 na kuwa katika mwaka huo hapakuwepo na taarifa za magonjwa
yaliyojitokeza ambayo yanazuilika kwa njia ya chanjo.
Aliongeza kuwa kuanzia Januari hadi Machi mwaka
huu wamewafikia na kuwapatia chanjo watoto 4806 kai ya watoto 4905 sawa
na asilimia 98 ya lengo kwa kipindi hicho kwa kuwachanja kwa magonjwa
dhidi ya Surua, pepopunda, porio, kifaduro, donda koo, homa ya ini, homa
ya uti wa mgongo na kichomi na kuwa kauri mbiu inasema "Jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya bora"
mmoja
wa akina mama aliyefika kupatia chanjo mwanae Ezra Njowela alisema
kujitokeza kupata chanjo hiyo kunatokana na mafunzo wanayopata tangu uja
uzito wanapohudhuria kliniki, hali inayofanya kujua umuhimu wa
kuhudhuria kliniki na umuhimu wa chanjo, hivyo kutambua faida za kuwachanja watoto wao na hasara ya kutochanja.
mwisho
No comments:
Post a Comment