Akiwasilisha salamu za Bodi ya Umoja wa Vyama
vya Wandishi wa Habari nchini Tanzania (UTPC) katika mkutano wa kwanza wa klabu ya waandishi
habari mkoani Songwe, mjumbe wa Bodi yake na mwenyekiti wa Klabu ya Wandishi wa
Habari Mkoa wa Iringa Frank Leonard alisema,
hali hii imekuwa ikikua siku hadi siku hivyo kuathiri ukuzaji wa upashanaji
habari
Alisema kuna wakati picha zinazowekwa
kwenye mitandao pamoja na habari zake zimekuwa zikidhalilisha watu, taasisi na
jamii hali ambayo imeendelea kupoteza msingi wa upatikanaji wa habari ambao ni
sehemu ya haki za msingi za kikatiba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
UTPC Abubakar Karsan alisema Songwe
imekuwa klabu ya kwanza ya wanahabari ikiwa imeanza na Kauli Mbiu yake isemayo "Ukweli Daima huponya Taifa" hatua
ambayo alisema ana matumaini nayo kutokana na namna wanavyojipanga
Aidha
aliongeza kuwa UTPC itatoa vifaa na kulipia gharama za uendeshaji wa
klabu kwa kipindi cha miaka kadhaa, hatua ambayo itajenga uwezo wa klabu
kujiendesha.
Mgeni rasmi aliyemwakilisha Katibu Tawala mkoani hapa Eliya Ntandu ambaye pia ni Katibu Tawala wilayani Mbozi Tusubilege Benjamin aliwaasa wanahabari mkoani Songwe kutumia vizuri fursa ya kukutana na watu mbalimbali katika kujiimarisha kiuchumi na kushiriki katika shughuli za kijamii badala ya kuhamasisha wengine kuondokana na umasikini huku wao wakibaki katika hali hiyo.
“ msitegemee tasinia hii kama chanzo pekee
cha mapato zitumieni vizuri fursa zilizoko, kwani ukiwa na uwezo hutanunuliwa
utafanya kazi yako ambayo ndiyo itakayokutambulisha kwa jamii yako”alisema
Aliwaasa wanahabari kujiepusha katiuka
kuingia katika makosa ya kijinai badala yake wasimamie ukweli daima kwa
kutanguliza uzalendo na utaifa kwanza.
Aidha katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa
Southern Garden Hotel mjini Vwawa wilayani Mbozi wajumbe walimchagua Stephano
Simbeye kuwa mwenyekiti wa muda wa Klabu hiyo kwa kura (21), Katibu Aines
Thobias, Makamu Mwenyekiti Zefrine Machesha, Mtunza Hazina Enea Mwanja na
wajumbe wawili Danny Tweve na Mecy Sekabongo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment