Social Icons

Tuesday, 19 September 2017

Songwe Waanzisha Klabu ya Wanahabari






Licha ya kuwa Mitandao ya kijamii kuwa vyanzo muhimu vya habari wakati huu duniani kote,   mapokeo kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania yamekuwa yenye mwelekeo hasi kutokana na taarifa zinazoripotiwa nyingi kati yake zimekuwa nje ya maadili ya jamii na habari kwa ujumla. 
 
Akiwasilisha salamu za Bodi ya Umoja wa Vyama vya Wandishi wa Habari nchini Tanzania (UTPC)  katika mkutano wa kwanza wa klabu ya waandishi habari mkoani Songwe, mjumbe wa Bodi yake na mwenyekiti wa Klabu ya Wandishi wa Habari Mkoa wa Iringa  Frank Leonard alisema, hali hii imekuwa ikikua siku hadi siku hivyo kuathiri ukuzaji wa upashanaji habari 

Alisema kuna wakati picha zinazowekwa kwenye mitandao pamoja na habari zake zimekuwa zikidhalilisha watu, taasisi na jamii hali ambayo imeendelea kupoteza msingi wa upatikanaji wa habari ambao ni sehemu ya haki za msingi za kikatiba. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC  Abubakar Karsan alisema Songwe imekuwa klabu ya kwanza ya wanahabari ikiwa imeanza na Kauli Mbiu yake isemayo  "Ukweli Daima huponya Taifa" hatua ambayo alisema ana matumaini nayo kutokana na namna wanavyojipanga
Aidha  aliongeza kuwa UTPC itatoa vifaa na kulipia gharama za uendeshaji wa klabu kwa kipindi cha miaka kadhaa, hatua ambayo itajenga uwezo wa klabu kujiendesha.
  
Mgeni rasmi aliyemwakilisha Katibu Tawala mkoani hapa Eliya Ntandu ambaye pia ni Katibu Tawala wilayani Mbozi Tusubilege Benjamin aliwaasa wanahabari mkoani Songwe kutumia vizuri fursa ya kukutana na watu mbalimbali katika kujiimarisha kiuchumi na kushiriki katika shughuli za kijamii badala ya kuhamasisha wengine kuondokana na umasikini huku wao wakibaki katika hali hiyo.
 
“ msitegemee tasinia hii kama chanzo pekee cha mapato zitumieni vizuri fursa zilizoko, kwani ukiwa na uwezo hutanunuliwa utafanya kazi yako ambayo ndiyo itakayokutambulisha kwa jamii yako”alisema 

Aliwaasa wanahabari kujiepusha katiuka kuingia katika makosa ya kijinai badala yake wasimamie ukweli daima kwa kutanguliza uzalendo na utaifa kwanza.

Aidha katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Southern Garden Hotel mjini Vwawa wilayani Mbozi wajumbe walimchagua Stephano Simbeye kuwa mwenyekiti wa muda wa Klabu hiyo kwa kura (21), Katibu Aines Thobias, Makamu Mwenyekiti Zefrine Machesha, Mtunza Hazina Enea Mwanja na wajumbe wawili Danny Tweve na Mecy Sekabongo.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment