Social Icons

Tuesday, 19 December 2017

Galawa Asitushwa Vikao Kuendelea Kuendeshwa kwa Makablasha



 Stephano Simbeye,

Mbozi: Mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku Galawa amemjia juu Meneja wakala wa barabara mkoa (Tanroads) kwa kuandaa kikao cha bodi ya barabara kwa kutumia makaratasi badala ya kutumia teknolojia ya tehama.

Galawa alisema hayo Jana akifungua kikao hicho ambacho kilifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi uliopo katika mji wa Vwawa kuwa hajafurahishwa na kitendo cha mkutano huo kuandaliwa kwa kutumia makabrasha wakati alipiga marufuku ili kupunguza matumizi ya fedha za serikari ili zipelekwe katika miradi mingine ya maendeleo.

Alisema anashangaa kuona wajumbe wa Bodi hiyo wanatumia makabrasha badala ya Tehama wakati wajumbe wengi walikwishagawiwa (ipad) ambapo makabrasha ya wajumbe yangetumwa kupitia humo na wajumbe wangekuwa wakitumia teknolojia hiyo kujadiliana.

Mkoa wa Songwe uliazimia kutumia teknolojia ya mawasiliano (TEHAMA) katika vikao vyake mbalimbali ili kurahisisha mawasiliano lakini pia kupunguza gharama kubwa iliyokuwa ikitumika kuandaa makabrasha na kuyafikisha kwa wajumbe katika vikao vya mabaraza ya madiwani ambapo kwa mwaka zinatumika zaidi ya Sh. 50 milioni.

Meneja wakala wa Barabara mkoani hapa Yohani Kasaini alisema kuwa alikiri na kusema kwamba hali hiyo haitajirudia tena kutumia makabrasha katika vikao vijavyo.

 ambapo pia alisema mkoa wa songwe kwa sehemu kubwa kuna changamoto ya miundo mbinu ambapo fedha inayotelewa ni ndogo ukilinganisha na uhitaji wa mkoa ambapo kwa mwaka 2017na 2018 mkoa wa songwe umetengewa bilioni 10. 1

mkuu wa wilaya ya momba juma saidi irando alisema kuwa anawaomba meneja wa TRD mkoan na TARURA wakafanye ukaguzi wa madaraja mawili yaliyojengwa katika harimashauri ya momba ambayo licha ya kujengwa hayatumiki na wananchi Huku yakionekana kujengwa chini ya kiwango.

Ubatizo japyon sonsa mwenyekiti wa harimashauri ya wilaya ya ileje amesema kuwa wakandalasi wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea ambapo wakati mwingine wanakaa nje na makambi yao na wakati mwingine kazi inasimama zaidi ya wiki mbili na kuvuka mda wa mkataba huku wananchi wakipata shida kubwa juu ya mawasiliano ya barabara ambapo pia alipendekeza barabara ya mpembe, isongole, kwenda kyela inatengenezwa ili kufungua mawasiliano kati ya wilaya ya kyela na ileje.

Ernest mgeni mratibu wa tarura mkoa wa songwe alisema kuwa kutokana na uchanga wa mkoa changamoto ni nyingi lakini atahakikisha anawasimamia vilivyo mameneja waliowekwa kila wilaya ili kurahisisha huduma kwa wananchi.

Aidha katika kikao hicho Galawa alisema kuwa wakuu wa wilaya ya Momba Jumaa Irando  wanachunguza kwa ukaribu wakandalasi waliopewa tends katika wilaya husika ili kuakikisha fedha za wananchi zinasimamiwa vizuri na kuwawajibisha wale watakaofanya kazi kwa mazoea

No comments:

Post a Comment