Social Icons

Monday, 19 September 2016

Na: Stephano Simbeye MKAZI wa kitongoji cha Mlamba kijiji cha Ilondo kata ya Malangali tarafa ya Bunda wilayani Ileje mkoani Songwe,Mussa Mshani (24),amefariki dunia kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali miguuni na kichwani hadi kufa na watu wasiofahamika na kuzuka kwa sintofahamu kwa wakazi wa eneo hilo. Akizungunza na waandishi wa habari ofisini kwake jana ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoani Songwe Mathias Nyange alisema tukio hilo lilitokea Septemba 18 mwaka huu katika kijiji hicho,ambapo jeshi lake lilifika eneo la tukio baada ya kupewa tarifa za mauaji hayo na wasamalia wema. Alisema walipofika eneo hilo la tukio walikuta mtu huyo amepigwa maeneo ya kichwani na miguuni hadi kufa na watu wasiofahamika ambapo waliruhusu ndugu na jamaa wa marehemu kuendelea na taratibu za maziko huku wao wakiendelea na taratibu za kiuchunguzi ili kuwabaini wahusika ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria. Alieleza kuwa chanzo cha tukio hilo bado hakijajurikana ambapo wanaendelea na upelelezi wa namna ya kuwabaini wahusika walioendesha mauaji hayo ya kinyama. Alisema mambo mengine ya kiuchunguzi juu ya tukio hilo watayawekwa wazi pindi watakapo kamirisha na kuwabaini wahusika na kuwa jeshi lake lipo makini kuhakikisha wahusika wote wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa hatua zaidi. Kamanda Nyange,alisema atahakikisha waharifu wote wanapatikana na kupelekwa kwenye vyombo vya kisheria na kuwa ametangaza hali ya hatari kwa watu wanaoendesha vitendo hivyo na kuwa Songwe ya sasa inatakawa kuwaa na watu wastaarabu na si wavunjifu wa amani ambao wanaharibu maisha ya wenzao kwa masirahi yao binafisi. Wananchi kwa upande wao wamesikitishwa na tukio hilo na kudai kuwa wameyapokea mauaji hayo kwa masikitiko makubwa na kuliomba jeshi la polisi kuwabana watu hao ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kupelekwa mahakamani ili iwe fundisho kwa watu wengine. Waliongeza kuwa watu hao wanaoendesha vitendo hivto vya mauaji au kuharibu maisha ya wengine wanatakiwa kusakwa popote walipo na vyomb vya sheria ili kuondoa kuwepo kwa vitendo hivyo visivyokuwa na tija. Ili kudhibiti hali ya matukio hayo ya mauaji,ipo haja ya serikali kuendesha semina elekezi kwa wakazi wa Ileje na wilaya zingine ndani ya mkoa wa Songwe ili jamii ione kuwa vitendo hivyo si vizuri na havimpendezi mungu. Mwisho.

No comments:

Post a Comment