VIONGOZI wa Baraza la wanawake la
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) wamekerwa na kitendo cha Serikali
kuwazuia wakulima kuuza mazao yao kwenye masoko ya nje ya nchi huku ikishindwa
kuwapunguzia bei ya pembejeo za ruzuku,
Viongozi wa baraza hilo,ambao pia ni
wabunge ni Risala kabongo,mbunge viti maalum mkoa wa Songwe,Hawa Mwaifunga viti
maalum Tabora,Kunti Yusuph viti maalum DododomaNagy Kaboyoka mbunge jimbo la
Same mashariki,walitembelea wilaya zote mkoani humo kuzungumza na wanawake
wenzao.
Viongozi hao,waliweza kuzungumza na
wanawake wenzao mambo mbalimbali pamoja na changamoto na kero
zinazowakabili na kupanga namna ya kupambana nazo ambapo waliahidi kuzipeleka
bungeni ili zikafanyiwe kazi.
Susan Simchimba,mkazi wa
Mbozi,alisema wilaya hiyo,imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo kuuziwa pembejeo
kwa bei kubwa ambazo ni feki huku mazao wanayoyapata japo ni kidogo wanapewa
masharti namna na mahara pa kuuzia mazao yao.
Asanga Juma mkazi wa Mbozi,alisema
changamoto kubwa inayowakabiri ni ukosefu wa fedha asilimia tano zinazotengwa
na serikali kwenye halmashauri kwa ajili ya wanawake na vijana licha ya kuwa
wameanzisha vikundi lakini wamekuwa hawapati fedha hizo.
Risala Kabongo mbunge viti maalum
mkoani Songwe,alisema ni kosa serikali kumpangia mkulima sehemu za kuuza mazao
yake wakati amelima kwa shida ili auze mahala atakapo ili aweze kupata fedha za
kuendeshea maisha kwa kuwa asilimia 75 wamategemea kilimo.
Alisem atakapo rudi bungeni
atazipeleka kero hizo ili zifanyiwe kazi,ikiwa ni pamoja na kuikumbusha
serikali kupunguza bei za pembejeo kwa kuwa walilizungumzia bungeni linasubili
utekelezaji na kuwa kuhusu asilimia 5 fedha za vijana na wanawake atazungumza
na wabunge wenzake ili zitolewe.
Nao wabunge viti maalum Hawa
Mwaifunga wa Tabora,Kunti Yusuph wa Dododma na Nagy Kaboyoka mbunge wa Same
mashariki,kwa nyakati tofauti,walisema wamezikusanya kero zote zinazowahusu
wanawake na kuwa wanaendelea kwenda maeneo mengineyo ili kupata kero na
wataziwakirisha bungeni.
Walisema wanawake wa mkoa wa Songwe
pamoja na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakikabiriwa na changamoto nyingi ambazo
zinahitaji usimamizi na ufuatiliaji,hivyo walisema wataungana na mbunge
mwenyeji Risala Kabongo kuziondoa changamoto za wananchi.
Baada ya viongozi hao wa Bawacha
ambao pia ni wabunge kuzunguka wilaya zote za mkoa wa Songwe baadaye
walimsindikiza mbunge mwenyeji ambaye aliitisha mkutano wa adhara jimbo la
Mbozi ambapo alizungumza na wananchi na kuchukua kero mbalimbali akiahidi
kuzipeleka bungeni.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment