Stephano
Simbeye, Mbozi
Mkuu wa mkoa wa
Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa amekemea vilali marumbano yanayoendelea ya
kuzusha uongo kuhusu mahali pa kujenga ofisi ya mkoa kuwa yanawachelewesha
kufikia malengo ya kujiletea maendeleo ya haraka ya mkoa.
Kauli hiyo
ameitoa leo alipokuwa akizungumza na madiwani katika kikao cha kupitia hoja za
mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) kuwa kumekuwa na vikao visivyo
rasmi ambavyo vimezua ubishani usiokuwa na afya na kudai kuwa mkoa unaiburuza
halmashauri ya wilaya kwa kubatilisha uamuzi wa awali wa maeneo
yaliyopendekezwa kujengwa ofisi za mkuu wa mkoa.
" waheshimiwa madiwani tunakoenda siko
tutachelewesha maendeleo ya wanasongwe na kuwa taratibu za kufikia hatua ya
maamuzi bado haijafikiwa maneno yanatoka wapi nawaasa acheni ubinafsi tufanye kazi kwa manufaa ya mkoa wetu"alihoji Galawa
Alisema hivi
sasa wataalamu wanapitia maeneo mengi ili kubaini fursa zilizopo na baadaye
vikao halali vitafanyika na kuwa zitashindanishwa hoja na vigezo na eneo
litakalokuwa na vigezo vinavyokubalika litapitishwa kwa utaratibu uliopo na si
vinginevyo.
Alisema kila mmoja ajiulize maswali muhimu
ambayo yatasaidia kuupeleka mbele mkoa kimaendeleo kwani maendeleo si jengo la
ofisi ya mkuu wa mkoa pia kuna vyuo vya ufundi stadi veta na shughuli nyingine
za uwekezaji. " alihoji
“Acheni kugombea
ofisi itajengwa wapi acheni wataalamu wabaineshe vizuri fursa za maeneo
zilizopo, na tuwe wamoja kuhakikisha tunakwenda salama, mimi niko hapa
nimeletwa nifanye kazi nitaondoka na wenye mkoa mtakaobaki mtakuja kumbuka
wakati mmekwishakosea na kujutia" alisema mkuu huyo wa mkoa
Akizungumza
wakati wa kufunga Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbozi Elick Ambakisye alisema
chanzo cha migogoro na ubishani huo unatokana na kuwapo baadhi ya viongozi
(hakuwataja) wanaofanya vikao na mikutano isiyo rasmi ambayo inajadili suala la
makao makuu pasipo kushirikisha wadau wengine.
“ Mheshimiwa
Mkuu wa mkoa kuna viongozi wenzetu
wanafanya vikao mbadala ambavyo vimekuwa vikituvuruga muda mrefu wilayani kwetu
kwa mfano tunasimamia sheria ya mazingira inyokataza kulima ndani ya mita
sitini, lakini kuna viongozi wenzetu wanakwenda kufanya mikutano ya hadhara na
kuwaambia watu walime ndani ya mita tano” alisema Ambakisye
Aidha kumekuwa
na mijadala miongoni mw wakazi wa Vwawa kufuatia taarifa kwamba serikali
inafanya mchakato wa kutafuta eneo linguine la kujenga makao makuu ya mkoa nje
ya maeneo matatu yaliypendekezwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment