VWAWA:Baadhi ya wakazi wa Jimbo la
Vwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe,jana walimtaka mbunge wa jimbo hilo, Japhet
Hasunga (CCM) kuwapa majibu ya sababu wilaya ya Mbozi kupata hati yenye mashaka
kwa miaka minne mfurulizo na kuwapa majibu ya hatua walizochukua dhidi ya
waliosababisha hali hiyo.
Wakizungumza jana kwenye mkutano wa
hadhara wananchi hao wakiongozwa na Jonson Nkota mkazi wa Ichenjezya, aliosema
amekuwa akifuatilia vyombo vya habari akisikia halmashauri ya Mbozi imepata
hati yenye mashaka kwa miaka minne mfurulizo lakini hajasikia hatua
zikichukuliwa kwa wahusika.
Alisema halmashauri za wilaya
zingine zimekuwa zikiwafukuza kazi wakurugenzi,maafisa utumishi,manunuzi pamoja
na watumishi wengine kutokana na kushindwa kuwajibika na ndiyo maana zimekuwa
zikipata hati safi lakini halmashauri ya Mbozi imegeuka shamba la bibi.
‘’Haiwezekani kila mwaka tupate hati
chafu wakati tunavyanzo lukuki vya mapato halafu hakuna hatua zinazochukuliwa
kwa wanaosababisha hali hiyo,tunakuomba mbunge ukae na wabunge wenzako mtupe
majibu sababu ya kupata hati chafu na hatua walizochukua kwa waliosababisha’’alisema
Nkota.
Akijibu hoja hizo,Mbunge wa jimbo la
Vwawa Japhet Hasunga alisema,hoja za wananchi ni sahihi lakini halmashauri
hiyo,imekuwa ikipata hati zenye mashaka miaka minne mfurulizo lakini si hati
chafu,na kuwa hati za mashaka ni zenye mapungufu.
Hasunga ambaye pia ni mjumbe wa
kamati ya bajeti katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania,alikiri kuwa
katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi,hali si shwari kitendo cha kupata hati za
mashaka ni tatizo wakati Mbozi ni tajiri lakini usimamizi si mzuri.
Alisema halmashauri zingine huo
zinathamanisha mali zake kila baada ya miaka mitatu lakini Mbozi haijawahi
kufanya hivyo ndiyo sababu ya kupata hati za mashaka na kuwa alitamani
kuhudhuria kikao kijacho lakini jumapili anakwenda Dodoma kupitia mahesabu ya
taasisi zote kupitia kamati yake.
Hasunga alimaliza kwa kuwaahidi
wananchi wa Mbozi kuwa suala la upatikanaji wa hati za mashaka katika
wilaya hiyo haitajitokeza tena na kuwataka wawe watulivu wazidi kuwaamini
wabunge wao pamoja na madiwani kwa kushirikiana na watendaji na kwamba
wamejipanga vizuri.
Aidha Edward Kalinga mkazi wa
Hasanga alisema taarifa za hati za mashaka zimekuwa zikiwaletea hofu kubwa hasa
ikizingatiwa kwamba kuna baadhi ya miradi ambayo fedha zilitolewa na hazikufanya
kazi iliyokusudia alitoa mano zaidi ya S. milioni 135 zilizotoea ka ajili ya
kujenga mabara lakini azikuanya kazi iliyokusudiwa
No comments:
Post a Comment