Social Icons

Wednesday, 19 October 2016

Bibi Kizee Akatwa mkono na vibaka kisha kukimbia nao





Na Ibrahim Yassin,Kyela

BIBI kikongwe mmoja Mkazi wa kijiji cha kanemele kata ya lusungo wilayani Kyela mkoani Mbeya Veronica Kanemele (75) amevamiwana watu  wasio  julikana  nyumbani  kwake   usiku wa manane  na  kukatwa mkono wa kushoto na kitu chenye  ncha kali kakutokana na  kile  kinachodaiwa  kuwa  ni  imani  za  kishirikina.

Mashuhuda  wa  tukio  hilo  walikiambia gazeti hili  kuwa  tukio hilo la kushangaza lilitokea usiku  wa  manane  wakati  bibi huyo  akiwa  amelala  fofo  nyumbani  kwake  , ambapo  bila  kujua hili  wala  lile  alijikuta akikatwa  mkono wake  wa  kushoto  uliopelekea   kunyofoka na  kusemawanashangaakutokana na  tukio    hilo  kuwa   la  kwanza  kutokea  maeneo  hayo.

Walisema baada ya kusikia bibi huyo akipiga mayowe ya kuomba msaada ndipo walijitokeza  waliamua  kutoa  taarifa  kwa mwenyekiti  wa  kitongoji   hicho  ambae  alifika mapema  na  kutoa  taarifa  kwa  uongozi   ngazi  ya  juu ambao ulifika  eneo  la tukio  na   kutoa  taarifa  polisi.

Akizungumzia tukio hilo   kwa masikitiko makubwa  mwenyekiti wa kitongoji cha Bugogo,Zakaria Ngasa  alisema baada   ya  kuwasili eneola  tukio alifanya jitihada za  kumkimbiza hospital ya  Matemakwa  ajili  ya  matibabu  kutokana na  kwamba mkono wake ulikuwa umekatwa na  kunig’inia na kupelekea  madakitari  kuunyofoa  mkono huo  baada  ya  kushindikana  kuungwa.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo,Veronika Kanyanyila alikirikutokea kwa tukio hilo na kusema kitendo hicho kimewasikitisha wananchi na ameitaka jamii kuliachia jeshi la polisi kufanya kazi yake na kuwasaka waalifu popote walipo ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Alisema  kijiji  hakiwezi  kuwashinda   watu  walio na imani  potofu za  kishirikina  na  kufanya  matukio  hayo , na  kuwaomba  wananchi kushirikiana  kwa  pamoja na jeshi la polisi  ili  kuweza  kuwanasa  watuhumiwa  na kufikishwa  kwenye  vyombo  vya   sheria .

Alisema  ifike  wakati watu  waweze  kumwogopa  mungu  kwani kufanya  vitendo hivyo kuna  fanya   watu  kuwa  na  hofu   husani wazee vikongwe kuishi  bila amani  kutokana na  uwepo  wa  matukio  hayo.

Mkuu wa jeshi la polisi wilayani kyela Amiri Mahamba alisema amepata taarifa ya tukio hilo na ametuma askari kwa ajili ya kuchunguza na atatoa ufafanuzi zaidi baada ya kupata taarifa za kina juu ya tukio hilo.
Kamanda wa polis mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jashi lake linaendelea na uchunguzi wa kuwasaka wahusika wa tukio hilo.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment