Stephano Simbeye
MBOZI:Wananchi mkoani Songwe wameaswa
kuepuka migogoro isiyo kuwa na tija badala yake waimalishe umoja na mshikamano
na kufanya kazi kwa bidii na maarifa kila mmoja kwa nafasi yake katika kuenzi
yale aliyo yapigania Mwl.Nyerere.
Wito huo umetolewa na leo na Mkuu wa Mkoa
wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa katika maadhimisho ya miaka 17 tangu
kufariki Mwassisi wa Taifa hili na Rais wa kwanza wa wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania hayati Julius Kambarage Nyerere iliyo fanyika mjini Vwawa wilayani
Mbozi Mkoa hapa kuwa wasipoteze muda kushughulikia mambo yasiyo ya msingi
Alisema kuendekeza migongano kutachelewesha
maendeleo,kwani badala ya kufanya kazi muda mwingi utapotea kushughulikia
migogoro jambo ambalo halitakuwa na tija yoyote bali kwa pamoja wajipange
kufanya kazi na wasikubali maneno ya kuwagawa.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kwa kulaan
watu wanao haribu mazingira kuwa hao hawalitakii mema Taifa hili kwani
uhalibifu wao utaleta jangwa ambalo litasababisha mvua ikakosekana.
Awali Mzee maarufu na ambaye Pia alikuwa
mwenyekiti wa kwanza wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Mzee Nelsen Mwampashe
amesema mfumo wa vyama vingi vya siasa ulianzishwa na Nyerere ili viweze
kuikosoa serikali iliyopo madalakani ili ijisahishe.
Naye
Mwenyekiti wa mamwene wilayani hapa Chifu Mleshelwa Nzuda alisema anamkumbuka Nyerere
kwa kuondoa ukabila ambapo alisema kabla ya hapo ilikuwa vigumu kabila lingine
kuja kulima katika ardhi yao jambo ambalo kwa sasa halipo tena, na kwamba yeye
kama chifu ana mke wa kabila lingine na wanaishi vizuri.
No comments:
Post a Comment