Stephano Simbeye, Mbozi
Wajumbe wa Baraza la Mamlaka ya mji
mdogo wa Vwawa jana waligoma kuendelea na kikao cha baraza hilo ikiwa ni
njia ya kushinikiza halmashauri ya wilaya Mbozi mkoani Songwe kurejesha zaidi
ya Sh. 126milioni ambazo zingejenga matundu 32 ya vyoo, vyumba sita vya
madarasa , ilizotumia bila ridhaa yake hivyo kufanya miradi hiyo kukwama .
Akizungumza mapema wakati wa
kuridhia ajenda za kikao hicho ambacho kilikua cha kawaida mmoja ya wajumbe hao Yaled Mtafya aliomba mwongozo
kuhusu utekelezaji wa maazimio ya baraza la dharura lililokaa Septemba 27
mwaka huu na kutoa maazimio ya kutaka hamashauri ya wilaya iwapatie kiasi hicho
cha fedha na kwamba isipofanya hivyo wajachukua hatuwa ya kurudi kwa wananchi
na kuwataka wasilipe tozo zozote za mamlaka hiyo hadi hapo fedha hizo
zitakapopatiana
Alisema kwa muda mrefu sasa mamlaka
ya mji haijafanya sughuli yoyote ya maendeleo kutokana na fedha za makusanyo
yake zimehodhiwa na halmashauri na jitihada za kufuatilia hazijazaa matunda
hali iliyofanya kamati ya fedha kwenda kwa mkuu wa wilaya ambaye naye
amedhalauliwa kutokana na kutotekeleza maagizo yake.
Mwenyekiti wa mamlaka ya mji wa
Vwawa Ephraim Mwakateba aliitaja baadhi ya miradi iliyokwama kutokana na
kukosekana kwa fedha hizo kuwa ni pamoja na ujenzi wa matundu 32 ya vyoo katika
shule za msingi za Ilolo na seondari Vwawa, vyumba viwili vya madarasa katika
shule ya msingi Mtumbo, vyumba vya madarasa 8 na ujenzi wa shule mpya ya kidato
cha tano katika kata ya hasanga na kazi ya uzoaji taka katika maeneo mbalimbali
ya mji.
Alisema chanzo cha mgogoro huo ni
agizo la serikali kutaka akaunti za mamlaka zifungwe na kuanza kuingiza
makusanyo yatokanayo na vyanzo vya mapato yake katika akaunti za halmasauri ya
wilaya jambo ambalo linaonesha halmashauri imezitumia fedha hizo kwa
matumizi mengine bila ridhaa ya wenye fedha hivyo kusababisha usumbufu
zinapohitajika
Mwakateba
Alisema azimio la kugoma kuendelea na kikao hicho linatokana na
kucheleweshwa kwa fedha za Mamlaka ambazo zilikuwa zikiingizwa kwenye
akaunti ya halmashauri kwa agizo la serikali na kwamba iwapo fedha hizo
hazitarejeshwa wanatoa
siku saba kwa halmashauri iwe imelipa fedha hizo vinginevyo watafanya
mikutano
ya hadhara kuwakataza wananchi wasitoe malipo yoyote hadi hapo suala
hili
litakapoisha na ikibidi watakwenda kumuona Waziri wa Tamisemi George Simbachawene
Akizungumza kwenye kikao hicho kabla
ya kuvunjika Afisa Mtendaji Mkuu wa mamlaka hiyo Joel Kaminyoge aliwataka
wajumbe hao kubadili msimamo wao kwani utekelezaji wa maazimio ya kikao chao
cha dharura cha Septemba 27 mwaka huu, umeanza baada ya halmashauri kuanza
kulipa fedha zao ikiwa ni pamoja na Sh. 26 milioni, malipo ya Sh. 18 milioni
yamekamilika na malipo mengine ya Sh. 8.8 yanakaribia kukamilika.
Kaminyoge alisema tofauti na huko
nyuma ambapo kwa mwezi zilikuwa zinalipwa Sh. 1 milioni kwa mwezi lakini sasa
kazi imeongezeka hivyo kuwaomba madiwani kusubiri hatua alizoanza kuzichukua.
“ waheshimiwa wajumbe tusubiri
kiongozi wetu akamilishe jitihada zake za kutusaidia kupata fedha zetu na hapa
mmesikia kuwa ameagiza kwamba kabla ya Novemba 4 mwaka huu awe amepelekewa
mchanganuo wa namna ya kulipa kwa maandishi” alisema Kaminyoge
Awali akitoa salamu za serikali Mkuu
wa wilaya ya Mbozi John Palingo aliwataka wajumbe wa Mamlaka ya mji kuzitumia
fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo ambayo hawajaitekeleza kwa muda wa mwaka
mzima.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment