Vwawa: Mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama
cha Mapinduzi (NEC) Taifa kutoka wilaya ya Mbozi mkoani Songwe George
Mwanisongole aliyeazimiwa kuvuliwa wadhifa wake huo hivi karibuni amejitokeza
hadharani na kudai kuwa sababu zilizodaiwa si za kweli na kwamba yaliyojitokeza
yana lengo la kumdhoofisha kisiasa.
Hayo yamejitokeza siku chache baada ya
wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Mbozi kumtuhumu mjumbe huyo wa NEC
pamoja na katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM) wilaya Yueni Kaminyoge waliokuwa
wakituhumiwa kwa kukigawa chama, kutoa siri za chama, na kusababisha aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Mbozi Godfrey Zambi kuanguka katika uchaguzi mkuu uliopita,
huku mwenezi akituhumiwa kwa kukiuka maadili ya uongozi kwa kulewa hovyo.
Baada ya kutumbuliwa Mjumbe huyo wa NEC
amejitokeza hadharani na kudai kwamba sababu zilizotolewa hazina ukweli wowote
bali kushindwa kwa Mbunge Zambi kulitokana na upepo wa mgombea Urais kupitia
Ukawa Edward Lowasa na yeye kutokubalika kwa wananchi, pia wakati huo wanaCCM.
“ mimi nilikuwa mgombea Ubunge katika kura
za maoni na nilishika nafasi ya pili, ningewezaje kuwashawishi wapiga kura na
kwanini nguvu hiyo nisingeepeleka kwenye kura za maoni ili kushawishi wajumbe
wanichangue” alihoji Mwenisongole.
Alisema tangu uchaguzi kwisha amekuwa
akifanya shughuli zake za kiuchumi na kuishi Jijini Dar es salaam hivyo kuwa
vigumu kuja wilayani kugawa chama, Hata hivyo Mwenisongole alisema tangu
Januari mwaka huu amekuwa akigawa vifaa vya
umeme jua 5000 kwa wakazi wa wilaya ya Mbozi karibu katika vijiji vyote jambo
ambalo pia limemfanya ajengewe uadui na wanasiasa wenzake ambao wamekuwa
wakiona kama anafanya kampeni za uchaguzi ujao.
Oktoba 19 mwaka huu wajumbe wa halmashauri
Kuu ya CCM wilaya waliazimia kuwa mjumbe wa NEEC taifa na Katibu wa Itikadi na
Uenezi wilaya waondolewe kwenye nyadhifa zao kwa madai ya kukigawa chama na
ulevi wa kupindukia.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbozi Aloyce
Mdalavuma alisema jambo hilo lilijitokeza katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM
wilaya ambao walitoa uamuzi ambao ulitolewa na wajumbe wenyewe na si uamuzi wa
mtu mmoja na kwamba kufuatia uamuzi huo hatua za kushughulikia jambo hilo kwa
kufuata taratibu zitafuata.
Alisema kwa mujibu wa taratibu suala hili
litapelekwe kwenye vikao vya kamati ya Siasa na hatimaye kurejeshwa tena kwenye
kikao cha halmashauri kuu wilaya kwa
maamuzi na kasha suala hilo kupelekwa katika ngazi ya mkoa na hatimaye taifa
kwa maamuzi ya mwisho.
Mwisho
Stephano Simbeye, Mbozi
Timu ya Kimondo SC ya Mbozi mkoani Songwe
inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania Bara, inakabiliwa na ukata wa fedha
ambao unafanya hali ya kambi ya wachezaji na viongozi wake kuwa ngumu huku
mashambiki wa mchezo huo wakinyoshewa kidole kwa kutoiunga mkono timu.
Wakizungumza jana katika hafla fupi ya
kukabidhiwa jezi zilizotolewa na Kampuni ya madini Shanta Gold Mine
iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Songwe mjini Vwawa baadhi
ya wachezaji walidai kwamba wanakabiliwa na uhaba wa mahitaji muhimu ikiwemo
chakula na fedha hali inayowafanya wachezaji kukosa ari.
Bruno Shayo ni mmoja wa wachezaji wa timu
ya Kimondo alisema timu ilijiandaa vizuri lakini changamoto iliyopo ni kuwa
mkoa haujaamka kimichezo ambapo wanashindwa kuiunga mkono timu hali
inayosababisha wajione wakiwa.
“ ligi ni ya kawaida haina ushindani
mkubwa lakini kikwazo ni pesa ambapo
wachezaji wanakabiliwa na uhaba wa posho za kujikimu jambo ambalo linatufanya tuwe
na mawazo mengi na kukosa molari ya kucheza mpira” alisema Shayo.
Golikipa wa Timu ya Kimondo Joseph Mwansile
aliwatupia lawama mashabiki wa mpira wilayani Mbozi kwa kushindwa kuiunga mkono
timu yao, hivyo hali kutokuwa tofauti wanapocheza nyumbani na ugenini.
Kapteni wa timu hiyo Abbas Athuman alisema
lengo la timu yao ni kupanda daraja ili icheze ligi Kuu msimu ujao lakini
wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa fedha na chakula.
Naye mkurugenzi wa timu ya Kimondo Elick
Ambakisye pamoja na kumshukuru Mkuu wa mkoa kwa Baraka zake kwa wafadhili
waliotoa vifaa hivyo lakini pia alisema timu inakabiliwa na uhaba wa rasilimali
fedha ambazo zinachangia kuharibu michezo.
“ mpera lazima unahitaji rasilimali fedha
ambayo ni changamoto kubwa katika timu yake na ambayo pia imekuwa ikivuruga
michezo kadhaa waliyocheza kutokana na timu washindani kuwavuruga waamuzi kwa
fedha na hivyo kutokuwa na maamuzi ya haki” alisema Ambakisye.
Kwa upande wake kocha mkuu wa timu ya
Kimondo SC Novatus Fulgence alisema wanaimarisha bechi la ufundi ili
kuhakikisha timu inafanya vizuri katika michezo iliyobakia ili kufikia mkakati
wao wa kupanda daraja na kucheza ligi kuu msimu ujao, licha ya kuwa timu
haijaanza vizuri katika michezo ya mwanzo.
Msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa
na Kampuni ya madini ya Shanta Gold Mine ni pamoja na Jezi jozi nne, mipira 4 na jezi za walinda
mlango jozi nane vyote vikiwa na thamani ya Sh.
900000
Akizungumza katika hafla hiyo mkuu wa mkoa
wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa aliwasihi wachezaji wa timu hiyo kujituma
katika mazoezi ili kufikia ndoto yao ya kushindana na wengine ili kupata
mafanikio.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment