Na: Stephano Simbeye, Chitete
MKUU wa wilaya Momba mkoani Songwe Bw.
Juma Irando amewata viongozi wa vijiji wilayani humo kutatua mapema migogoro ya
wakulima na wafugaji na kujiepusha kuwa sehemu ya tatizo kwa kushawishika na
tamaa ya fedha,kabla haijaleta madhala ya uvunjifu wa amani.
Alisema hayo jana wakati alipokuwa
akitowa salamu za serikali katika kikao cha baraza la madiwani katika mji wa
Chitete kuwa migogoro mingi ya wakulima na wafugaji husababishwa na viongozi wa
vijiji na kata baadae inakuwa shida hadi kwenye ngazi ya wilaya.
“ kumekuwa na migogoro ya hapa na
pale hasa ya wakulima na wafugaji tusingependa kuona migogoro hii ikiendelea na
kukua bali ishughulikiwe na kumalizwa mapema pia wafugaji wasio na vibali
wasiruhusiwe kwani hawa ndiyo chanzo cha migogoro” alisema mkuu huyo wa wilaya.
Bw. Irando alisema mkoa unaandaa
wasifu wake ikiwemo kurasimisha ardhi yake, hivyo isingekuwa vizuri kuacha watu
wengine wakiuza ardhi yao wengine wakihamahama maeneo bali jitahidini kwa nguvu
zao zote kulisimamia jambo hilo.
Mmoja wa wakulima katika kijiji cha
Nkara Bw. Erasmus Sinkamba alisema kumekuwa na baadhi ya viongozi wa vijiji na
kata kurubuniwa na wafugaji kwa kupatiwa fedha ili kutoa ardhi kwa wafugaji
ambao pia wamekuwa wakilisha mifugo yao kwenye mazao ya wakulima.
Alisema katika maneo yao tatizo hilo
bado halijashamili lakini ni vizuri likachukuliwa tahadhari mapema kwani katika
maeneo jirani wilayani humo tayari limekwisha anza ambapo wafugaji
wanaingia na makundi makubwa ya mifugo yao wakisaka malisho na maji.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya hiyo alisema Bw. Vedaestani
Simpassa aliwasihi madiwani na watendaji kutekeleza maagizo hayo na
shughuli nyingine kwa bidii na kusahau siasa ambazo muda wake umekwisha bali
wakati huu ni kutekeleza yaliyo mbele yao ili kuhakikisha wilaya yao inakuwa
salama na inakwenda mbele kimaendeleo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment