Na: Stephano Simbeye - Songwe
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Songwe inatarajia kuendesha midahalo katika wilaya
zote, itakayowahusisha wananchi na wadau mbalimbali kuzungumzia kero za
wananchi kuhusu rushwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maadili na
haki za binadamu itakayofikia kilele Desemba 10 mwaka huu.
Mkuu wa Takukuru mkoani hapa
Emmanuel Kiyabo aliwaambia waandishi wa habari jana katika kikao kilichofanyika
katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa mjini Vwawa kuwa, maadhimisho ya mwaka
huu yatafanyika katika awamu mbili, ambapo Desemba 5 hadi desemba 8 mwaka huu
katika ofisi za TAKUKURU wilaya za Ileje, Mji wa Tunduma na katika ofisi ya
mkoa iliyopo Vwawa wilayani Mbozi zitasikiliza kero za wananchi dhidi ya rushwa.
Alisema awamu ya pili itahusisha
midahalo itakayofanyika siku ya kilele Desemba 10 mwaka huu ambayo pia
imeandaliwa na ofisi za Takukuru wilaya zote, ambapo katika ofisi ya mkoa mjini
Vwawa kutakuwa na mdahalo wa vijana wa Scouts ambapo patafanyika mjadala
utakaongozwa na mada isemayo “ maadili na ruswa” pia mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa Mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni Mtsafu Chiku Galawa.
Kiyabo aliongeza kuwa huko katika
wilaya ya Ileje kutafanyika mdahalo ambapo mjadala utahusu mada isemypo“kero za
usambazaji wa pembeeo za ruzku” ambapo ofisa kilimo wilyani humo atakuwepo
kujibu hoja zinazohusu ugawaji wa pembejeo za ruzuku, na katika mji wa Tunduma
mdahalo utauwa na mjadala usemao “ je rushwa na ukosefu wa maadili vinachangia
uwepo wa migogoro ya ardhi?|”
Mkazi wa Hanseketwa wilayani Mbozi
Israel Swila alisema kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kuripoti masuala
ya rushwa litakuwa jambo muhimu kwani watu wengi hawajui namna na wapi mahali
pa kuwasilisha kero zao has wanapoombwa rushwa ndogongogo huko vijijini waliko.
Alisema katika maeneo ya utoaji
huduma kama vile ofisi za watendaji wa vijiji na kata, na mabaraza ya kata kuna
ukandamizaji mwingi ambao unasababishwa na wananchi wengi utoelewa sheria
mao9fisa wa maeneo husika wanatumia mwanya huo kuwanyanyasa wananchhi kwa
kuwatoza rushwa.
Fatuma Mwanyula mkazi wa Nambala
alisema makongamano hayo yasingoje kipindi cha maadhimisho ndipo yafanyike bali
uwe utaratibu wa kila wakati ili kuwaelimisha wananchi juu ya hai zao na wajibu
wao kwa ujumla ili wafahamu namna ya kuepuka kutoa rushwa na kutoa ushirikiano
kwa mamlaka husika pale wanapoombwa au kuona viashiria vya rushwa.
“wakati mwingine tunafanyiwa urasimu
katika huduma pasipokuombwa kitu lakini ukilitizama suala lenyewe utagundua
kuwa kinachotafutwa ni kitu kidogo ili upate huduma, kwa mfano suala la
ugawaqji wa mbolea za ruzuku baadhi ya watendaji huandika majina bandia ili
kunufaika na baadaye kuchukua pembejeo hizo kwa manufaa yao wenyewe.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment