Stephano Simbeye,Mbozi:
Wakazi watatu wa kijiji cha Ipanzya kata ya Ipunga wilayani Mbozi
mkoani Songwe jana walipandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Mbozi
kujibu shitaka la kuchoma moto nyumba yenye thamani ya Sh. 1.2 milioni mali ya Wastafily
Mwamlima kinyume na kifungu cha sheria namba 329 kanuni ya adhabu sura ya 16.
Ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi Diventini
Nyahoro kuwa tukio hilo lilitokea septemba 11 mwaka jana saa 7 usiku, washitakiwa
hao walivamia nyumba na kuichoma moto na kumjeruhi mwenye nyumba kwa makusudi
bila halali huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Aliwataja Washitakiwa hao kuwa ni Obedi Luoga (51) ,Mwashuma Mwamlima
(47) , Salum Abdala (32) wote wakiwa wakazi wa kijiji hicho
Aidha Nyahoro aliongeza kuwa nyumba hiyo yenye thamani ya sh. milioni
moja na laki mbili iliyochomwa na washitakiwa hao na kumjeruhi mlalamikaji
sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia kisu huku wakijua kufanya hivyo ni
kosa kisheria.
Hata hivyo washitakiwa wote walikana shitaka hilo mbele ya hakimu wa
mahakama hiyo Nemes Chami ambaye pia aliahirisha
shauri hilo mpaka January 17 mwaka huu na washitakiwa wote wameachiwa kwa
dhamana, kwa sharti la kuwa na wdhamini wawili kila mmoja na mali
isiyohamishika.
Mwisho
No comments:
Post a Comment