Stephano Simbeye, Mbozi,
VWAWA: Serekali ya Tanzania na Zambia zimesaini mkataba wa
makubaliano ya kuanzisha kituo cha pamoja cha
mpakani Tunduma na Nakonde nchini Zambia kwa lengo la kupunguza urasimu
mpakani na kurahisisha ufanyaji biashara n a upitishaji wa mizigo mpakani.
Akizungumza mara
baada ya zoezi la kuweka saini Naibu Katibu mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Amina Shaaban alisema
kukamilika kwa mpango huo ni utekelezaji wa agizo la marais Dr. John Pombe Magufuli na rais Dr. Edgar
Lungu wa Zambia alipofanya ziara hapa nchini ambapo walikubaliana kituo hicho
mkianze kufanya kazi mara moja.
Alisema katika kufanikisha makubaliano hayo yametiwa saini
na Makatibu Wakuu wa nchi hizi mbili wakiwa ni Makatibu wakuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango na Wizara ya viwanda na uwekezaji wa Tanzania na Makatibu
Wakuu wa wizara za biashara na viwanda, maendeleo ya nyumba na miundombinu na
Jimbo la Mchinga wa Zambia ambao walikutana katika kikao cha pamoja
kilichofanyika mjini Vwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Shaaban alisema pamoja na makubaliano ya kuanza kufanya kazi
kwa kituo cha pamoja cha Tunduma/Nakonde, viongozi hao pia wamesaini mwongozo
wa utendaji pamoja na mfumo wa
urahisishaji biashara kati ya nchi hizo mbili.
0763274634
Alisema hiki kitakuwa ni kituo cha tano kwa upande wa
Tanzania ambapo vituo vingine ni pamoja na Holili-Taveta katika mpaka wa
Tanzania na Kenya, Rusumo (Tanzania na Ruanda), Mutukula (Tanzania na Uganda),
na Kabanga/Kobela (Tanzania na Burundi).
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na
Uwekezaji wa Tanzania Prof. Adol Mkenda alisema kusainiwa kwa mkataba huo
kutasaidia kurahisisha ufanyaji biashara mpakani kwa bidhaa zile zinazotambuliwa
pande zote bila usumbufu naMpango kumaliza biashara za magendo mpakani.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Jamhuri
ya Zambia Kayula Siame alisema maubaliano hayo yanafungua ukurasa mpya wa ushirikiano kwa kuwa shughuli
katika kituo zitafanyika kwa uwazi katika kituo kimoja.
Aidha alisema makubaliano hayo yatasaidia kuongeza mapato
kwa pande zote na kukomesha biashara ya magendo ambayo inapoteza mapato ya
serikali zote mbili na pia kuhatarisha usalama mpakani.
Aliongeza kuwa hiki kitakuwa kituo cha pili cha mpakani
kikitanguiwa na kile cha Chilundu katika mpaka wa Tanzania na Zimbabwe.
Naibu Kamishina wa Mamlaka ya mapato Tanzania Charles
Kicheele alisema ofisi yake imejiandaa kikamilifu kuanza kwa shughuli za pamoja
mpakani ambapo kwa sasa wamekarabati jingo lililopo ili kuanza kazi mapema wiki
ya kwanza ya mwezi Februari mwaka huu wakati kazi ya ujenzi wa jingo jipya
ikiendelea.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment