Stephano Simbeye, Mwananchi
TUNDUMA: Maduka sita yameteketea kwa moto katika soko la
Manzese katika halmashauri ya mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe
kutokana na hitilafu ya umeme na kusababisha hasara kubwa.
Mmoja ya wamiliki wa maduka jirani na yaliyoungua Itika
Mwashibanda akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi alisema
kwamba moto huo ulianza kuwaka saa sita usiku wa kuamkia leo ambapo unasadikiwa
kuwa chanzo chake ni hitirafu ya umeme
Alisema hata hivyo kutokana na jitihada za wananchi kwa
kushirikiana na jeshi la polisi na kikosi cha zimamoto cha Nakonde Zambia
walifanikiwa kuuzima moto huo.
Geradi Donard ni shuhuda aliyekuwepo wakati moto huo
unazimwa alisema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umemeambapo umekuwa
ukikatwa mara kwa mara na kurejeshwa kutokana na kuhamisha nguzo za umeme ili
kupisha upanuzi wa barabara unaoendelea katika mji huo.
Alisema hili ni tukio la pili la kuteketea kw maduka ya
wafanybiashara ambapo tukio kama hilo lilitokea maka jana na kuteketeza maduka
matatu, hata hivyo wamekuwa wakipata msaada toka kikosi ch zimamoto kutoka nchi
jirani ya Zambia na kuuzima moto huo.
Kamanda wa Polisi mkoani Songwe Mathias Nyange amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi bado unaendelea ili kubaini chanzo
cha moto huo na pia bado thamani halisi ya mali zilizoteketea haijafahamika na
hakuna madhara kwa binadamu.
Kamanda nyange ametowa wito kwa wafanyabiashara kote mkoani
Songwe kuzima vifaa vyote vya umeme wanapofunga maduka yao ili kuepusha
hitilafu inayoweza kutokea.
Mwisho
No comments:
Post a Comment