Wafanyabiashara na wadau mbali mbali
wa elimu wilayani mbozi mkoani Songwe wameombwa kutoa misada katika shule
zilizopo wilayani hapa ili kuipunguzia mzigo serikali kwani haiwezi peke yake
kumaliza changamoto zilizopo katika jamii.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Edna Mwaigomole wakati akipokea fulemu tano
zenye thamani ya zaidi ya sh. Laki 5 za shule ya msingi Nuru iliopo vwawa
wilayani hapa kutoka kwa mdau wa elimu Exaud Kajela.
Mwaigomole ameongeza kuwa msaada
ambao umetolewa na mdau huyo utasidia kupunguza changamoto zinazoikabili shule
ya nuru ambayo ni mpya na haina milango wa fulemu za madirisha.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada
huo Exaud Kajela amesema kuwa amesukumwa kuchangia fulemu hizo baada ya kupata
taarifa kutoka kwa mwalimu kuwa kuna changamoto wakati wa kufundisha wakati
mvua zikinyesha hivyo uelewa kwa wananfunzi unakuwa tatizo kubwa.
Kwa upande wake afisa elimu ufundi
wilayani Mbozi Nobati Kisimba kuna uhitaji wa madarasa 2242 lakini vilivyopo ni
1228 kwa iyo kuna upungufu wa madarasa 967 na upungufu utazibwa na shule 10
zinazojengwa wilayani hapa na tano kati ya hizo zitakazokamilika mapema
zitaanza mwaka huu.
Naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Nuru Fausta Nzunda akitoa maelezo ya awali katika hafla hiyo alisema shule hiyo
ilianza mwaka 2013 ikiwa ni mchepuo kutoka shule mama ya Haloli baada ya
kufulika wanafunzi, imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya vyumba vya madarasa
hali inayofanya wanafunzi warundikane katika vyumba vichache vilivyopo na hivyo
kutosoma vizuri.
Kufuatia changamoto hiyo wananchi
waliamua kujenga vyumba vitatu vya madarasa tangu mwaka 2014 kwa gharama ya Sh.3.09milioni,
nayo halmashauri ya wilaya ya Mbozi ilitoawa Sh. 4.03milioni ili kuunga mkono
jitihada za wananchi, ofisi ya Mbunge wa jimbo la Vwawa ilitowa 2.150milioni
hata hivyo majengo hayo bado hayajakamilika hali iliyofanya waanze kutafuta
wadau wa kusaidia na ndipo walipompata Exaudi Kajela.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment