Stephano Simbeye,
Vwawa:
Chama cha walimu Tanzania
(CWT) kimeanza kugawa mipira ya michezo mbalimbali mashuleni kwa ajili ya
kuhamasisha walimu kuunda timu ikiwa ni hatua ya kuhamasisha wafanye mazoezi
ili kuboresha afya zao.
Katibu wa chama hicho wilayani hapa
Herbet Mkonjera akiongea wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mipira 60 jana kwa
ajili ya walimu wa shule za msingi na sekondari alisema kuwa mipira hiyo
imetolewa na Naibu Katibu mkuu wa CWT Taifa Ezekiel Ouloch kwa lengo la
kuwafanya walimu waunde timu zao za michezo mbalimbali ambayo itakuwa ni hatua
ya kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan la kuwataka
watanzania kufanya mazoezi.
Aliwataka walimu kupanga ratiba ya
mazoezi na ikibidi kuwa na mashindano na shule nyingine, ama na waratibu ambao
nao wamepatiwa mipira yao ili waunde timu yao.
Akizungumza kabla ya kukabidhi
mipira hiyo Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya mbozi George Mwakapala alisema
zoezi la kutoa mipira kwa walimu litakuwa endelevu kila mwaka na kuwa chama
hicho kinakusudia kuunda timu moja ya wilaya ambayo itatokana miongoni mwa
wachezaji watakaokuwa kwenye timu za shule.
‘tunataka mwisho wa siku timu ya
wilaya tuipandishe daraja hadi icheze ligi kuu tokea mkoa wa Songwe, hata hivyo CWT haikuangalia mpira wa miguu tu
bali ni pamoja na mpira wa mikono na pete pia“alisema Mwenyekiti huyo
Mmoja wa wawakilishi wa walimu Victoria
Kibona alisema mipira hiyo itatumika kwa ajili ya
michezo ya walimu tu kuimarisha afya zao na kuwa pia kitendo cha walimu kuanza
kucheza pia kitachochea michezo kwa wanafunzi nao kuanza kuibua vipaji vyao
Sadrick
Mwashilindi ni mjumbe wa CWT wilaya anayewakilisha kundi la vijana alisema
kupitia michezo kutawaweka walimu katila mshikamano zaidi na hivyo kutimiza
lengo la kuanzishwa kwake la kiws na sauti moja
Mwisho
No comments:
Post a Comment