ILEJE: Mwanamke mmoja mkazi wa
kijiji cha Igumila wilayani Ileje mkoani Songwe Yeska Mlungu (50) amejeruhiwa
vibaya baada ya kukatwa mapanga na mume wake kwa madai ya kutompakulia nyama
aliyoinunua.
Shuhuda mmoja ambaye pia ni jirani
wa familia hiyo Lukas Swila alisema wa tukio hilo lilitokea juzi ambapo walisikia
kelele za mama huyo kuomba msaada na walipofika walikuta amepoteza fahamu huku
akitokwa na damu nyingi kutokana na majeraha aliyokuwa nayo.
Alisema baada ya hapo kwa kushirikiana na majirani wengine
waliitaarifu polisi ambao walitowa fomu ya matubabu (PF3) na kwenda hadi kwenye hospitali ya wilaya ya
Ileje (Itumba).
Akielezea tukio hilo Mama huyo katika hospitali ya Itumba alisema chanzo cha ugomvi wao ni nyama ambao mume wake huyo aitwaye aliinunua, lakini kutokana na kuwa ilikuwa kidogo aliwapakulia watoto na mume kukosa
Mganga wa zamu wa hosptali ya
Itumba Samsoni Wangwi alisema alimpokea majeruhi huyo akiwa na hali mbaya iliyotokana na kuvuja damu
nyingi kutokana na kupata majeraha makubwa.
Naye kaimu mganga mfawidhai wa
hosptali ya Itumba Damas Banzi alisema kuwa baada ya kuanzishiwa matibabu hali
ya majeruhi inaendelea vizuri na kwamba mwanaume huyo kitendo alichofanya ni ukatili
ambao unatakiwa kupigwa vita na elimu kutolewa kwa wanaume wenye tabia kama
hiyo.
Banzi aliongeza kuwa kwa sasa
wanajitahidi kumpatia matibabu mama huo ili kuurudisha mwili wake katika hali
yake ya kawaida licha ya kuwa amejeruhiwa vibaya.
Kamanda wa polisi mkoani
Songwe,Mathias Nyange,alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa
ametorokea kusiko julikana baada ya kutenda tukio hilo jana saa mbili usiku na
jeshi lake linaendelea kumsaka.
Aliongeza kuwa mashirika binafsi na
jamii kwa ujumla inatakiwa kushirikiana ili kupiga vita vitendo hivyo na
kusema kuwa wao kama jeshi la polisi watasimama kidete kupinga vitendo hivyo na
kuwafikisha kwenye mikono ya sheria wale wote ambao
wanawapiga na kuwanyanyasa wa wanawake.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment