Stephano Simbeye, Mwananchi
ssimbeye@mwananchi.co.tz
Tunduma: Mkuu wa wilaya ya Momba
Mkoani Songwe Juma Erando amewataka watumishi wa serikali wanaomiliki vyombo
vya moto kuingia darasani kusomea udereva ili wapate uhalali wa kuendesha
vyombo hivyo.
Kauli hiyo aliitowa Jana katika siku
ya hitimisho ya mafunzo ya waendesha pikipiki alimaarufu (boda boda) Yaliyo
fanyika Mji wa Tunduma uliopo wilaya ya Momba Mkoani Songwe.
Alisema kumekuwa na watumishi wengi
wa Serikali wanao miliki magari yao na kuyaendesha pasipo na mafunzo yoyote na
kuwa kufanya hivyo inaweza ikawa chanzo cha ajari zinazo tokea Barabarani kila
siku.
Juma aliwasistiza wahitimu wanao
maliza mafunzo ya udereva pikipiki (Boda boda) kuto kuvunja sheria zirizo wekwa
pamoja na maandamano au kutumika kisiasa. Pia katika hitimisho la mafunzo hayo
Mratibu na mkufunzi wa mafunzo ya usalama Barabarani kutoka Shirika lisilo la
kiserikari APEC Peter John Peter.
Ameiomba Serikali kuwapatia wahitimu
wa mafunzo hayo bima ya afya pamoja na kuwapatia Leseni mapema bila vikwazo
vyovyote. Mwisho
Mwisho.
No comments:
Post a Comment