Stephano Simbeye,
Jeshi la Polisi mkoani Songwe linawashikiria watu sita (6)
wakazi wa wilaya tatu za Mbozi, Ileje na Momba mkoani Songwe, baada ya kukutwa
wamelima bangi katika mashamba yeknye
ukubwa wa hekari 10.1/2 wakiwa wamechanganya katika mashamba yao waliyolima zao
la mahindi kinyume cha sheria.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Mathiasi Nyange alisema watu
hao walikamatwa katika msako wa matumizi ya dawa za kulevya unaoendelea nchini
kote ambapo jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu wawili wenye umri wa miaka
41 na 53 (majina yamehifadiwa) wakazi wa
kijiji cha Shaji kata ya Mlangali wilayani Mbozi akiwemo Mwenyekiti wa
kitongoji, wakiwa wamepanda bangi katika shamba lenye ukubwa wa hekari tano
huku ndani yake likiwa limechanganywa na mahindi.
Alisema katika tukio lingine katika kijiji cha Zelezeta kata
ya Igamba wilayani Mbozi mtu mmoja mwenye umri wa miaka 35 alikamatwa akiwa
anamiliki shamba lenye ukubwa wa hekari 2 na Iyua robo eari, wakati huko katika
wilaya ya Ileje katika kijiji cha Mbebe mtu mmoja alikutwa na shamba lenye
ukubwa wa nusu hekari na katika kijiji cha Chipaka wilayani Momba mtu mmoja
alikutwa na shamba lililopandwa bangi hekari mbili na nusu.
Nyange alisema watuhumiwa
hao wanatarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote na msako dhidi ya walima
bangi ni endelevu hadi watakapohakikisha hakuna tena ulimaji wa zao hilo mkoani
hapa, pia ametahadharisha viongozi wa vijiji ambao wanafumbia macho walimaji wa
bangi ambapo ameapa kuwachukulia hatua za kisheria.
Mwenyekiti wa kijiji cha Shaji Goodwell Haonga akizungumzia
tukio la mkazi wa kijiji hicho kukutwa na shamba la bangi alisema anashangazwa
na hali hiyo kwani mwanakijiji huyo makazi na mashamba yake viko pembeni kidogo
na makazi yaw engine hivyo inakuwa vigumu kuona na kutambua hali hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Mbozi John Palingo akizungumzia operesheni
hiyo alionya watu wanaolima bangi waache kufanya hivyo kwani mkono wa serikali
ni mrefu utawabana na watajikuta pabaya na badala yake walime mazao
yanayokubalika.
mwisho
No comments:
Post a Comment