Stephano Simbeye, Mbozi
Abilia wanne waliokuwa wakisafiri kwa Basi la New Force lenye namba T220 DPQ linalofanya safari zake kati ya Tunduma na Dar Es salaam wamejeruhiwa kufuatia basi hilo kupinduka leo asubuhi katika kijiji cha Chimbuya wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Mmoja wa abiria aliyenusulika katika ajali hiyo Adamu Kinyekile amesema ajali hiyo imetokea saa 12.20 asubuhi na kuwa chanzo cha ajali hiyo ni baada ya lori moja lililokuwa mbele ya basi hilo kusimama ghafla na kukata kona kuelekea upande wa kulia hali iliyofanya dereva wa basi hilo kushindwa kusimama na hivyo kukata kushoto ambako gari liliacha njia na kupinduka.
Akisimulia chanzo cha ajali dereva wa gari hilo Patrick Sanga alisema alikuwa ameongozana na lori ambapo gari lake lilikuwa katikati huku nyuma yake alikuwa akifuatwa na basi lingine mali ya kampuni hiyo na ghafla lori lilisimama na kukata kulia, lakini kutokana na hali hiyo aliamua kukata kushoto ili asiligonge kwa nyuma ambapo ingesababisha madhara makubwa.
“ nilipoamua kusimama ghafla na mimi na kukata kushoto kwa bahati mbaya magurudumu ya nyuma yalipita kwenye nyasi na wakati huo ilikuwa asubuhi nyasi zina umande, hivyo magurudumu hayo yaliteleza na kulazimisha gari kuacha njia” alisema Patrick.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa Mathias Nyange amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha bali kuna abiria wane ambao wamepata majeraha madogomadogo.
Aidha Kamanda nyange alisema uchunguzi wa awali wa Polisi umebaini chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi aliokuwa nao dereva ambao ulisababisha ashindwe kulimudu gari lake.
Mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment