Na: Mwandishi wetu Mbozi:
Baadhi ya wananchi wa mkoa
wa Songwe wamesema wana matumaini ya kuboreshewa miundombinu ya barabara na
fursa ya kufanya biashara katika kipindi cha uzinduzi wa mbio za Mwenge wa
Uhuru kitaifa mwaka huu utakaofanyika April 2 mwaka huu.
Mkazi wa kijiji cha
Idiwili William Mwahalende alisema kwa kuwa hii ni mara ya kwanza tukio kama
hilo kufanyika katika mkoa huu, ni vizuri Serikali ikaelekeza nguvu zake katika
kuboresha miundombinu ya barabara na
madaraja ambazo nyingi hazipitiki katika kipindi hiki cha masika.
Mkazi wa Vwawa Mbwiga
Mwampashe alisema tukio hilo ni la kihistoria kwa wilaya ya Mbozi na mkoa wa Songwe
kwa ujumla, hivyo wamejiandaa kuitumia fursa hiyo kufanya biashara hivyo
kuongeza kipato chao kwa kuuza bidhaa mbalimbali ikiwemo vyakula.
Aidha mwampashe alisema kuwa serikali imewatendea mambo mema
wana songwe ambapo kwa mwaka huu
wamepata waziri mwenye dhamana ya kilimo, kwa ujumla ni jambo la
kushukuru mungu.
Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoani hapa Yohana
Mwajeka alisema wafanyabiashara wamejipanga kutumia nafasi hiyo kufanya
biashara katika kipindi chote cha maandalizi ya uzinduzi wa Mwenge na hadi
kufikia siku yenyewe.
Mkuu wa mkoa wa Songwe Brigedia Jeneral Nicodemus Mwangela
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana aliwaomba wananchi
kushiriki katika tukio la uzinduzi wa mbio za Mwenge kitaifa kwa kuonyesha
umoja, mshikamano na uzalendo, ambapo alisema hiyo ni fursa pekee ya kuutangaza
mkoa na fursa zake za kiuchumi zilizopo.
Sambamba na fursa hizo pia alisema itakuwa ni mara ya kwanza
mwenge kuwashwa katika mikoa ya nyanda za juu kusini husuani mikoa ya Mbey
,Songwe ,Iringa,Rukwa ,Njombe na Katavi kwa zaidi ya miaka 10 iliyo pita.
Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema kabla ya uzinduzi huo
kufanyika yatafanyika makongamano ambayo yatatoa fursa kwavijana kujadili mambo
mbalimbali yanayohusu maslahi ya Taifa, ikiwa ni pamoja na uzalendo na namna
ambavyo Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere alikuwa mfano wa kuigwa kwa uzalendo
wake.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment