Stephano Simbeye,ILEJE:
Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kanda ya nyanda za juu kusini umeshauriwa kuanzisha
maeneo ya vivutio vya watalii ndani ya hifadhi ili kuwezesha kuwepo utalii wa
misitu kwa kuweka vituo vya kupumzikia
(Camping site) ili kukuza sekta ya utalii katika mikoa hiyo.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri Maliasili na Utalii
Japheti Hasunga alipokagua msitu wa Iyondo Mswima wenye ukubwa wa hekta 12053 uliopo
wilayani Ileje mkoani Songwe kuwa serikali imedhamilia kukuza sekta ya utalii
na hasa katika ukanda wa kusini ambao sekta hii haikutiliwa mkazo miaka mingi
ili kuongeza watalii wengi na pato la Taifa.
Alisema katika mikoa hiyo vipo vivutio vingi vya utalii ambavyo pia
havijabainishwa vinavyoweza kufanya utalii katika mikoa hiyo na kufanya
wananchi wakapata ajira na wakapiga hatua katika maisha yao.
“ Nawashauri bainisheni vivutio vilivyopo ili viwekewe
mkakati mahususi wa kuvitangaza na sambamba na hilo hamasisheni wafanyabiashara
kujenga mahoteli mazuri ya kitalii pamoja na kumbi za mikutano ili watalii
wakija wapate sehemu ya kulala, lakini pia wahamasisheni waanzishe makampuni ya
kuongoza watalii ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto fani za kuongoza watalii”
alisema Hasunga
Hasunga alisema kwa kuanzia katika eneo la hifadhi ya msitu
wa serikali wa Iyondo Mswima na mingine
wakala wa huduma za misitu wabuni njia ya kufanya ili kuanzisha utalii wa
misitu ambao unaweza ukawekewa vivutio vingine kama utamaduni wa asili ili
kuwafanya watalii kuvutika na hivyo kukaa muda mrefu katika maeneo hayo na
kuongeza kipato na ajira kwa wananchi.
Aidha aliongeza kuwa serikali imeanzisha mradi mkubwa wa
kufufua utalii katika Ukanda wa Kusini na kuongeza idadi ya watalii wanaoingia
nchini kutoka watalii 1489 mwaka jana hadi kufikia watalii zaidi ya 2800
ifikapo 2020 na kuongeza pato litokanalo na utalii kutoka dola za kimarekani
2bilioni hadi dola za kimarekani 5bilioni.
Awali akiwasilisha taarifa Meneja wa Msitu wa Iyondo Mswima
Ibrahimu Msinga msitu huo umetowa ajira kwa watu 400 katika msimu wa upandaji
miti na kwamba mwaka huu unatarajia kuongeza ajira za watu 250 baada ya
shughuli kuongezeka kwa ajili ya kuhudumia bustani ya miti na kazi ya upandaji.
Aidha alisema wakala huo umetowa miti 300 kwa halmashauri ya
wilaya ya Ileje kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwa wananchi ili kuimarishja
mahusiano mema baina ya wananchi na wakala huo(TFS) hata hivyo alisema ipo
changamoto ya wananchi kuingilia eneo la misitu ambapo wamepanda miti yao
binafsi katika eneo la zaidi ya hekta 40.5 kutokana na maeneo hayo kuwa wazi
muda mrefu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ileje
Ubatizo Songa alisema kutokana na kuanzishwa kwa hifadhi yam situ huo
halmashauri yake itaangalia namna ya kupanua wigo ili kufanya wilaya inufaike
na wananchi wake waweze kuongeza kipato kupitia misitu na utalii.
Alisema katika wilaya hiyo vipo vivutia vingi vya utalii
ambavyo havijatangazwa kama wanyama aina ya Mbega ambao ni adimu hapa nchini
lakini wanapatikana wilayani humo, maanguko ya mito ambayo pia yanaweza kuwa
vivutio lakini kutokana na kutoitangazwa vivutio hivyo havijawanufaisha.
Mmoja wa wakazi wa kata ya Sange ulipo msitu huo Sailas
Kibona alisema kutokana na hali ya hewa na mazingira ya eneo walilolopo ya safu
nyingi za milima, anaamini linaweza kuwa kivutio kikubwa cha utalii hivyo
kuwanufaisha kwa kupata ajira na kipato.
Alisema pia uwepo wa kisitu katika eneo lao umechangia kwa
sehemu kubwa kuwapatia kipato kwani katika maeneo yao ardhi kwa ajili ya kilimo
cha mazao ni kidogo hivyo wanatumia misitu kujiongezea kipato kwa kupasua mbao
na kuziuza.
Kwa upande wake Katibu Tawala wilayani humu Mary Joseph
alisema kitendo cha serikali kuu kupitia wakala wa hifadhi ya misitu Tanzania
kuanzisha mradi katika wilaya hiyo utasaidia kuibadilisha wilaya ya Ileje
kutoka hapo ilipo sasa na kuwa yenye uchumi mkubwa katika kipindi cha miaka 20
ijayo na kuwa wilaya yenye viwanda vin gi vya mbao na kukuza pato la wilaya.
Alimuomba Naibu Waziri Maliasili na Utalii kuangalia pia
msitu wa asili wa Kyosa uliopo wilayani humo ambao kwa hivi sasa unakabiliwa na
uharibifu mkubwa ili kuona namna ambavyo serikali kupitia wakala wa huduma za
misitu ili kuuhifadhi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Aidha katika mkoa wa Songwe vipo vivutio vingi ikiwemo
Kimondo cha Mbozi, mapango ya popo, chemichemi za maji moto, unyayo wa binadamu
katika jiwe, matanuru ya kale na vingine vingi ambavyo iwapo vitawekewa mkazo
vinaweza kusaidia kuinua utalii katika ukanda huu.
Mwisho.
habari, samahan naomba mawasiliano ya uongozi wa shamba la miti la iyondo mswima lililotembelewa na makamu wa rais.
ReplyDeletenahitaj kutuma maombi ya kazi.
nahitaj email au namba ya mfanyakazi yeyote wa hapo
Naomba mawasiliano namna ya kufika
DeleteMbona hamjaweka mawasiliano kama mtu anataka kufika hasa kuona maji moto au vivutio hivyo? Naomba mawasiliano
ReplyDelete